Magufuli ataka Airtel kurejeshwa serikalini

RAIS John Magufuli amemuagiza Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango kufuatilia Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Airtel ili kujua ukweli ili umiliki wake urudi serikalini kabla ya kuisha kwa mwaka huu.

Alisema hayo jana katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), inayojengwa katika eneo la Makulu mjini hapa. Rais Magufuli alimuagiza Waziri wa Fedha na Mipango kufuatilia suala hilo haraka ili Airtel irudishwe kumilikiwa na serikali. “Fuatilia suala la Airtel, Airtel kwa taarifa tulizonazo ni mali ya TTCL (Kampuni ya Simu Tanzania).

Palifanyika mchezo wa hovyo, sasa sitaki kuzungumza mengi fuatilia. “Nchi hii ilikuwa ya maajabu sana unachukua share (hisa) leo, kesho inauzwa, kisha zinafutwa na kuuzwa juu kwa dola moja,” alisema Rais Magufuli. Taarifa kuhusu Airtel Taarifa za kuaminika kutoka serikalini, zinaeleza kuwa TTCL itamiliki hisa zote za Airtel Tanzania Limited, ambapo tayari TTCL imewasilisha hoja ya kutaka kufanya hivyo baada ya kubaini kwamba serikali ilipunjwa kwenye hesabu za uwekezaji.

Inaelezwa kuwa hoja ya Airtel kuwa mali ya TTCL inaanzia Novemba 3, 1998, ilipoanzisha kampuni tanzu ya Cellnet ambayo ilifanya kazi mpaka Mei 7, 2001 ilipobadilishwa jina na kuitwa Celtel Tanzania, huku umiliki wake ukiendelea kuwa chini ya shirika hilo kwa asilimia zote baada ya kuwekeza dola milioni tano za Marekani (zaidi ya Shbilioni 11). Inaelezwa kuwa Januari 31, 2002, Celtel ikiwa chini ya umiliki wa TTCL ilikopa dola 82 milioni (zaidi ya Sh bilioni 180.4) ili kukuza mtaji wake.

Kwa kipindi hicho, TTCL iliyokuwa na thamani ya dola 600 milioni (zaidi ya Sh trilioni 1.32) ilikuwa inamilikiwa kwa ubia kati ya Serikali na Kampuni ya Mobile System International (MSI) ya Uholanzi. Serikali ilikuwa inamiliki asilimia 65 ya hisa zote na mbia huyo asilimia 35 zilizosalia. Agosti 5, 2005, mabadiliko yalifanywa kwenye Bodi ya Wakurugenzi wa Celtel kwa lengo la kuunda kampuni mbili tofauti; Celtel ikatenganishwa na TTCL.

Kutokana na mabadiliko hayo, Celtel iliwekwa chini ya umiliki wa MSI ambayo Septemba 2007 iliuza hisa zake kwa Zain, ambayo nayo ilikuja kuziuza kwa Bharti Airtel Juni 8, 2010. Imeelezwa kuwa TTCL inadai uwekezaji wake ilioufanya Celtel baadaye Airtel, ambayo thamani yake imeongezeka maradufu sasa, haulingani na inachokipata, hivyo kutaka kusimamia biashara za kampuni hiyo ya mawasiliano.

Hoja ya madai hayo ni namna umiliki wa hisa ulivyobadilishwa baada ya Celtel kutenganishwa na TTCL, ambayo ilipewa hisa chache, tofauti na ilivyostahili. Kwa sasa, Airtel Tanzania inamilikiwa na Serikali yenye asilimia 40 na Celtel Tanzania BV, kampuni tanzu ya Zain Africa BV ambayo ilinunuliwa na Bharti Airtel International, Novemba, 2010 ikiwa na asilimia 60.

Katika mabadiliko yaliyofanywa hivi karibuni, Serikali iliilipa Bharti Airtel Sh bilioni 14.7 hivyo kuchukua asilimia 35 ya hisa ilizokuwa inamiliki na kuifanya imiliki asilimia zote za TTCL. Sheria mpya iliyopitishwa hivi karibuni na Bunge, imeibadili TTCL inayohudumia asilimia 0.82 ya soko kuwa shirika la umma la mawasiliano na kulipa jukumu kubwa katika sekta ya mawasiliano nchini.

Bharti Airtel inatakiwa kuorodhesha asilimia 25 ya hisa zake katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) ili kukidhi vigezo vya Sheria ya Posta na Mawasiliano ya mwaka 2010, lakini haijafanya hivyo. Onyo kwa watoa takwimu za uongo Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ametoa onyo kuwa hatua kali zitachukuliwa na mamlaka husika kwa mtu yeyote atakayetoa takwimu za uongo kwa lengo la kupotosha umma.

Alisema kwa mujibu wa Kifungu cha Sheria 37 ya Mwaka 2015 Namba 3 hadi 5, adhabu kali zitachukuliwa kwa mtu atayehusika kutoa taarifa za uongo, ikiwa ni pamoja na kufungwa jela miezi sita au miaka mitatu au kulipa faini ya Sh milioni moja au adhabu zote kwa pamoja. “Nawaomba Watanzania, kwa mtu yeyote atayehitaji takwimu za kitu chochote, akachukue kwa mamlaka husika,” aliagiza Rais Magufuli.

Pia alisema uchumi wa Tanzania unakua, ambapo katika nusu ya kwanza ya mwaka huu umekua kwa asilimia 6.8, mfumuko wa bei umeshuka hadi kufikia asilimia 4.4 mwezi Novemba 2017 na akiba ya fedha za kigeni imefikia dola za Marekani bilioni 5.82, ambayo inaiwezesha nchi kununua bidhaa na huduma miezi mitano, ikilinganishwa na wastani unaopaswa wa miezi minne.

“Mpaka sasa Tanzania imeweka Sh bilioni 5.8 ya akiba ya fedha za kigeni na Sh bilioni 2.5 zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya vituo vya mkoa wa Dodoma,” alisema. Alisema pia kwa muda wa miaka miwili, jumla ya viwanda vipya 336 vimejengwa. “Serikali imetenga kiasi cha Sh bilioni 23 kwa kila mwezi kwa ajili ya kutoa elimu bure na mpaka sasa asilimia 31 ya wanafunzi hujiunga na kidato cha kwanza,” alisema Rais Magufuli.

Pia aliwataka Watanzania kupuuza msemo wa kuwa ‘vyuma vimekaza’, badala yake kuangalia takwimu zinasema nini kuhusu uchumi wa Taifa. “Kwa wale wanaolalamika vyuma vinabana, wajue vitaendelea kubana tumbo, vitabana kichwa na hata viungo vyote vya mwili,” alisema Rais Magufuli. Awali, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Twakimu (NBS), Dk Albina Chuwa alisema kwa mujibu wa takwimu za Taifa, matarajio ya mwaka 2022, idadi ya Watanzania itaongezeka mpaka kufikia milioni 61.3.

“Tanzania ni nchi ya pili barani Afrika baada ya Afrika Kusini katika ukusanyaji wa takwimu bora, tumeendelea kutoa mafunzo kwa watakwimu katika taasisi za serikali ili kuendana na mabadiliko katika eneo la takwimu,” alisema.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mpango alisema ujenzi wa ofisi hizo ni agizo la Rais Magufuli la kuhamisha shughuli za serikali Makao Makuu Dodoma. Msomi azungumzia hisa za Airtel Kutokana na agizo hilo la Rais Magufuli kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mpango, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Benson Bana alisema linapaswa kuungwa mkono.

Alisema kumekuwa na michezo ya hovyo kwa miaka ya hivi karibuni kwa baadhi ya makampuni na mahoteli, kubadilisha majina kinyemela, hali inayoleta wasiwasi kwamba ni moja ya njia za ukwepaji kodi.

Profesa Bana alisema kuwa Rais anavyo vyombo vyake, ambavyo vinampa taarifa nyingi, hivyo maagizo yake kwa Waziri wa Fedha ni sahihi. Kwa upande mwingine, baadhi ya wachumi waliozungumza na gazeti hili walisema hawawezi kutoa maoni yoyote, kwa kuwa agizo hilo linamtaka Waziri kulifanyia kazi. Walisema kwa kuwa suala lenyewe, pia ni la kimikataba na la kisheria, hivyo ingefaa watu wawe na uvumilivu, kuona ni kitu gani Dk Mpango aliyeagizwa kufuatilia, atakuja nacho.

Source: www.habarileo.co.tz

Ramaphosa ahaidi kuimarisha uchumi wa Afrika Kusini

Kiongozi mpya wa chama cha ANC cha Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amefunga rasmi mkutano wa chama hicho akiahidi kufanyia kazi sera za kuimarisha uchumi wa nchi hiyo.

Akizungumza katika kikao kilichomalizika usiku wa manane, Ramaphosa amesema kupambana na rushwa sambamba na umaskini ni kipaumbele cha kwanza kwa chama chake.

Amesema kuwa kikao cha kamati kuu kimeahisi pia kurudisha ardhi muhimu ambazo zilikua mikononi mwa wasiohitajika ikiwa ni lengo la kukuza sekta ya kilimo.

Amemsifu mpinzani wake wa kaziribu ayembwaga kwenye kinyang’anyiro cha uenyekiti wa ANC Nkosazana Dlamini Zuma kuwa ni jasiri na mchapa kazi.

source: www.bbc.com

Uganda yaondoa kikomo cha umri wa kugombea urais

Wabunge wa Uganda wameyapitisha mabadiliko ya Katiba ambayo sasa yanamruhusu Rais wa sasa Yoweri Kaguta Museveni kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa kwa muhula wa sita.

Baada ya siku tatu za majadiliano mazito na mivutano, hatimaye waondoa ukomo wa umri wa miaka 75 kwa mgombea urais. Wabunge wa upinzani walitoka ndani ya ukumbi zaidi ya mara moja na sita kati yao walifukuzwa ukumbini kutokana na kuupinga muswada. Na hatimaye spika wa bunge hilo Bi Rebecca Kadaga akitangaza matokeo baada ya kupiga kura ya mwisho ikiwa wapiga kura wawili hawakuwa na upande, upinzani wamepata kura 62 na wanaotaka kuondowa kikomo kura 315 na hivyo Spika kutangaza kuwa mswaada huo umepita baada ya kusomwa mara ya tatu.

Wabunge pia wamerejesha ukomo wa vipindi viwili vya kukaa madarakani kutoka miaka saba hadi miaka mitano, kwa hivyo wabunge wa sasa wataendelea kuongoza hadi mwaka 2023.

Ni pengine kutokanana malalamiko kuwa kuondolewa kwa ukomo wa umri kunaweza kumfanya Bwana Museveni kuwa Rais wa milele. Wafuasi wa Museveni wanadai ni waganda ndiyo wanaweza kumwondoa madarakani kwa Kura.

Upande wa upinzani waliweka pingamizi kuzuia mswaada huo usipite lakini idadi yao katika bunge ni ndogo, kiongozi wa wabunge wa upinzani Winne Kiiza amesikitishwa na kupitishwa mswaada huo.

Lakini upande wa chama tawala ulitumia kila mbinu kuona kwamba mswaada huo unapita ili Rais Museveni kuendelea kutawala .

Kupitishwa mswaada huo kunampatia tena Rais Museveni kutawala miaka mingine 14 kulingana na mswaada huo, lakini raia wa Uganda wengi walikuwa hawaungi mkono kubadilishwa kwa katiba kumuongeza Rais Museveni kutawala baada ya kutawala zaidi ya miongo mitatu.

Source: www.bbc.com

Korea Kusini yaitaka Marekani kusitisha mazoezi ya kijeshi nchini humo

Marekani na Korea Kaskazini zimekuwa katika mgogoro wa muda mrefu kufuatia mpango wa matumizi ya mabomu ya nyuklia unaofanywa na Korea Kaskazini.

Michuano ya Olimpiki ya majira ya baridi inatarajiwa kuhusisha pia wanamichezo kutoka Korea Kaskazini jambo ambalo Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In anaeleza kuwa ni la kuimarisha uhusiano zaidi.

Source: www.bbc.com

Wasambaza uongo Bakwata kukiona

BARAZA Kuu la Waislamu nchini (Bakwata) Mkoa wa Dar es Salaam limesema kuwa watu wote waliosambaza taarifa za uongo na uchochezi kuhusu Mufti na Shehe Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir pamoja na baraza hilo watachukuliwa hatua kwa kuwa wanafahamika.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Shehe Mkuu wa Mkoa huo, Alhad Mussa Salum wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa hizo zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari. Kauli hiyo imekuja baada ya hivi karibuni katika mitandao mbalimbali ya kijamii ilisambaa taarifa kuwa mfumo wa baraza hilo kiutendaji hauko imara na wana mkakati wa kumpindua Zubeir.

“Kwa hakika tunawajua hawa ambao wamelianzisha hili na Mufti anawajua na mimi ninawajua na mufti atawashughulikia hivi karibuni kwa kuwa waliotengeneza ni watu wachache waliomo ndani ya baraza,” alisema Salum.

Alisema Waislamu kote nchini wanapaswa kupuuza taarifa hizo kwa kuwa ni za uongo na zina lengo la kudhoofisha baraza na jitihada za Mufti za kuokoa na kuzilinda mali za baraza na kulijenga upya ili liweze kujitegemea na kujiendesha lenyewe kiuchumi na kuwaunganisha Waislamu wote nchini kuwa kitu kimoja bila kujali tofauti zao kiitikadi.

“Hakuna shehe yeyote kwetu sisi mashehe wa mikoa kama wasaidizi wake ambaye hana imani na mufti kama inavyodaiwa na hakuna mjumbe yeyote wa Baraza la Ulamaa ambaye hana imani na mufti wala mashehe wa wilaya hasa ukizingatia kwa muda mfupi mambo ambayo ameyafanya,” aliongeza. Aidha, Salum alisema kuwa Bakwata ni baraza ambalo linajitegemea na siyo tawi la Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama taarifa mbalimbali katika mitandao ya kijamii zinavyodai.

Source: www.habarileo.co.tz

Reli ya Tanga-Arusha iliyokufa miaka 14 yafufuliwa

SERIKALI imesema imeanza kufufua reli ya kaskazini ya kutoka Tanga hadi Arusha, ambayo ilikufa miaka 14 iliyopita.

Lengo la hatua hiyo ni kuwezesha wafanyabiashara na wananchi, kusafirisha mizigo yao kwa kutumia reli hiyo badala ya barabara, hatua itakayopunguza uharibifu wa miundombinu ya barabara nchini.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alipokuwa akikagua ukarabati wa reli hiyo kuanzia eneo la Korogwe hadi Mombo, ambalo limekamilika kwa kilometa 83.

Aliwahakikishia Watanzania kuwa uendelezaji wa reli hiyo hadi Arusha, utakamilika Aprili mwakani, hivyo kuruhusu huduma za usafirishaji ziendelee hasa za mazao na bidhaa. “Niwahakikishie wananchi kuwa hii kazi tuliyoianza haiwezi kusimama kwani serikali imejipanga na itaendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri za usafirishaji,” alisema Mbarawa.

Alimtaka Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa, kuongeza ajira kwa vijana wa maeneo hayo. Aliwataka kuwa na uzalendo katika ukarabati wa reli hiyo ili kurahisisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kuhusu ‘bomoabomoa’ katika maeneo ya hifadhi ya reli, Profesa Mbarawa alisisitiza kuwa ataendelea kusimamia sheria kama inavyosema.

Aliutaka uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), kutafuta mizigo ili kuongeza huduma za usafirishaji wa mizigo kwani ukarabati wa njia hizo za reli, unahitaji fedha nyingi, hivyo upatikanaji wa mizigo hiyo utasaidia kuzalisha faida ambayo itawezesha kuongeza mapato ya shirika hilo.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO, Masanja Kadogosa, alisema kuwa ukarabati wa reli hiyo, utakuwa na mchango mkubwa kiuchumi na kijamii, kwani utasaidia kwa wananchi na wafanyabiashara kusafirisha mizigo yao kwa njia rahisi. Ukarabati wa reli hiyo yenye urefu wa kilometa 438 ni mkakati wa Serikali katika kufufua huduma za usafiri wa treni nchini na kufungua fursa za kiuchumi na kibiashara kwa wananchi.

Source: www.habarileo.co.tz

Magufuli: Four reasons why CCM won in 42 wards

Chama cha Mapinduzi (CCM) National Chairman Dr John Magufuli has outlined four reasons why the ruling party emerged the winner in the just ended councillorship race.

Opening CCM’s 9th General Assembly in Dodoma, Monday morning, Dr Magufuli, who doubles as the President, said that the party won in 42 wards out of 43 in the by-elections of councilorship since it has strong support from its members. Another reason that led the CCM to scoop the wards, leaving one to opposition Chadema, according Dr Magufuli, is an experience of the ruling party in the country’s politics for 40 years.

“We are implementing practically want we have promised,” cited the CCM national chairman as he was mentioning reasons why the party won. The fourth reason is that CCM has unity and solidarity among members hence it was a strong factor why the oldest party continues winning in every election over other competitors, he added.

Meanwhile, the chairman asked members of CCM who were vying various posts to dissolve their camps and support the winners in a bid to make the party stronger and stronger. “Losers shouldn’t feel bad. They should try again.

But they should support the winners and dissolves their affiliation groups,” he added. Secretary General (SG) Abdulrahiman Kinana added that the party’s internal democracy is another secret weapon for the CCM to remain in its winning ways in various elections.

Source: www.dailynews.co.tz

Tanzania yaongeza maradufu panya buku wanaotambua TB

Tanzania inaongeza maradufu idadi ya panya buku wanaotumika kuutambua ugonjwa wa kifua kikuua.

Panya hao hupewa mafunzo na wana uwezo wa kunusa kamasi za binaadamu na kutambua kwa haraka ugonjwa wa TB.

Wana uwezo wa kutambua sampuli mia moja kwa muda usiozidi dakika 20.

Tofuati na binaadamu – wataalamu wa maabara wanaotumia siku nne kuchunguza idadi hiyo ya sampuli.

Tanzania sasa itawatumia panya hao katika kliniki zipatazo 60 kote nchini.

Mfumo huu wa kutumia panya kutambua TB ulianzishwa na shirika la misaada Ubelgiji, kama njia nyepesi na na isiyotumia fedha nyingi kutambua TB kinyume na mfumo uliozoeleka.

Katika baadhi ya mataifa kusini mwa jangwa la Sahara, zaidi ya 50% ya wagonjwa wa TB hawatambuliwi au hawatibiwi na kote duniani, idadi hii ni ya juu kiasi cha milioni 4.1.

Kutotambuliwa kwa wagonjwa hawa wanaojumuisha watu wasiojiweza, na wasioweza kupata matibabu – wazee kwa vijana, watu wanaoishi katika umaskini, wachimbaji migodi na hata wahamiaji.

Iwapo mgonjwa hatopata matibabu, mgonjwa TB anaweza kusambaza ugonjwa huo kwa hadi watu 15 kwa mwaka.

Tanzania ni mojawapo wa mataifa 30 ambako kunashuhudiwa maambukizi makubwa ya kifua kikuu, ambao ni ugonjwa mmojawapo hatari unaosambaa kwa kasi na kuua watu, lakini unaoweza kutibiwana kuzuiwa.

Source: http://www.bbc.com

Tanzania yajitenga na Trump kuhusu Jerusalem

Tanzania imesema haikubaliani na hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania kupitia taarifa imesema nchi hiyo inaunga mkono makubaliano ya kimataifa ambayo yanatambua haki ya watu wa Palestina kumiliki Mashariki mwa Jerusalem kama ilivyokuwa kwenye mpaka wa kabla ya mwaka 1967.

“Tanzania inaunga mkono msimamo wa Umoja wa Mataifa wa suluhu ya mataifa mawili ambayo unatoa nafasi ya Israel na Palestina kuwepo kwa pamoja zikiwa na mipaka salama,” taarifa hiyo iliyotuwa saini na Waziri Augustine Mahiga imesema.

Bw Trump kando na kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel, alisema nchi hiyo pia itahamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv.

Bw Mahiga amesema ubalozi wa Tanzania utaendelea kuwepo mjini Tel Aviv.

Msimamo wa Tanzania unaenda sambamba na msimamo wa mataifa mengi ya Afrika pamoja na Tume ya Umoja wa Afrika (AU).

Mwenyekiti wa tume hiyo Moussa Faki alikuwa ametahadharisha kwamba hatua ya Trump “itaongeza uhasama kanda hiyo na hata maeneo mengine na kutoa changamoto zaidi katika juhudi za kutafuta suluhu ya mzozo wa Israel na Wapalestina.

Alisema Umoja wa Afrika unaendelea kuwaunga mkono Wapalestina na juhudi zao za “haki za kuwa na taifa huru ambalo litakuwa na Jerusalem Mashariki kama mji wake mkuu.”

“Hatua hii inatishia sio tu Mashariki ya Kati bali pia inachokoza ulimwengu woye wa Waislamu. Tunahofia kwamba hatua hii haitaathiri sio tu Afrika vibaya, bali pia itaifanya hali, ambayo kwa sasa inahitaji suluhu ya maiafa mawili, kuwa mbaya zaidi kuliko awali,” alisema Bw Faki.

Jumatano, mataifa 57 ya Kiislamu yalitoa wito kwa Jerusalem Mashariki kutambuliwa kama mji mkuu wa Wapalestina.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alikuwa ameyahimiza mataifa hayo katika mkutano mkuu wa muungano wa nchi za Kiislamu (OIC), kufanya hivyo akisema hatua ya Marekani ya kuutambua mji huo kama mji mkuu wa Israel ni “batili”.

Bw Erdogan pia kwa mara nyingine aliishutumu Israel na kuiita “taifa la kigaidi”.

KIongozi wa Wapalestina Mahmoud Abbas amesema Marekani “imejiondoa kutoka kwa kuwa mhusika mkuu katika shughuli ya kutafuta amani”.

Hadhi ya mji wa Jerusalem imekuwa sehemu ya mzozo wa Waisraeli na Wapalestina.

Kwa nini Jerusalem inazozaniwa?

Mji huo una maeneo matakatifu ya dini tatu zenye kufuata imani ya Ibrahim – Uyahudi, Ukristo na Uislamu – sana maeneo mengi yanapatikana Jerusalem Mashariki.

Israel ilitwaa eneo hilo kutoka Jordan wakati wa vita kati ya nchi za Kiarabu na Israel mwaka 1967 na imekuwa ikiuchukulia mji wote kuwa mji wake mkuu ambao hauwezi kugawanywa.

Jerusalem Mashariki hutazamwa kuwa mji mkuu wa taifa la Wapalestina (litakapoundwa) na mataifa ya Kiarabu na Kiislamu pamoja na Wapalestina wenyewe.

Kwa mujibu wa maafikiano wakati wa mazungumzo ya amani ya Wapalestina na Waisraeli ya 1993, hatima ya mji huo ilifaa kuamuliwa wakati wa hatua za mwisho za mazungumzo.

Source: http://www.bbc.com

Social security fund members reassured

PRESIDENT John Magufuli yesterday clarified on the government’s decision to merge pension funds in the country, assuring workers that their benefits won’t be affected.

The President said the government arrived at the decision in order to increase efficiency in the social security sector and improve the welfare of the members. “Nothing will be deducted from your benefits after merging the pension funds,” President Magufuli said at the opening session of the Tanzania Teachers’ Union General Meeting held in Dodoma.

President Magufuli said the country had many pension funds, prompting a scramble for members, a trend that contravened social security scheme procedures. “We want to have only two pension funds, one for the public and the other for the private sectors; the National Social Security Fund (NSSF) will remain as it is while the remaining pension funds would be merged to serve public servants,” President Magufuli said.

He said the move would also help to avoid forgery and fast track the payment of benefits. “Some pension funds had been using members’ contributions to invest in non-beneficial projects to safeguard their personal interests… this is corruption,” the President said. He said the government decision aimed at having social security schemes that were focused on safeguarding the interests of its members.

President Magufuli stressed that the pension funds should invest in industries which would create employment opportunities and earn the government revenue. He noted, however, that teachers and other stakeholders were still having a chance of airing their views to improve some sections because the bill was still at the early stage.

The President further said that the government had also paid a total of 1.3 trn/- out of 1.5 trn/- owed by social security schemes. In September this year, the government officially announced to merge five pension funds out of the current seven in order to improve services as well as be beneficial to the members.

The Deputy Minister in the Prime Minister’s Office (Policy, Parliamentary Affairs, Labour, Employment and the Disabled), Mr Anthony Mavunde, said that the pension funds would be merged in order to improve services. He said the government had collected views from various stakeholders on how to improve the social security industry. Mr Mavunde said the decision to merge the funds would be endorsed by the Cabinet in the near future.

Last month, a Minister in the Prime Minister’s Office (Policy, Parliamentary affairs, Labour, Employment and Disabled persons) Jenista Mhagama, said the envisaged merger would be undertaken carefully to avoid confusion amongst members. She also said that the government had started reviewing the 2003 social security policy in order to make sure that more people were covered.

“The current policy is very old; we want to make some amendments that would enable us to see various changes in the social security industry, she noted. According to the Social Security Regulatory Authority (SSRA), the country currently has seven social security funds — National Social Security Fund (NSSF), PPF Pension Fund, Public Service Pension Fund (PSPF), Local Authorities Pension Fund (LAPF), Workers’ Compensation Fund (WCF) , Government Employees Provident Fund (GEPF) and National Health Insurance Fund (NHIF), which offer similar benefits.

Stakeholders have been engaged to air their views on the envisaged trimming of social security schemes from the current number to either one or two to reduce the costs of pension benefits and operating costs.

Source: www.dailynews.co.tz