Entries by deborah01

Magufuli ataka Airtel kurejeshwa serikalini

RAIS John Magufuli amemuagiza Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango kufuatilia Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Airtel ili kujua ukweli ili umiliki wake urudi serikalini kabla ya kuisha kwa mwaka huu. Alisema hayo jana katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), inayojengwa katika […]

Ramaphosa ahaidi kuimarisha uchumi wa Afrika Kusini

Kiongozi mpya wa chama cha ANC cha Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amefunga rasmi mkutano wa chama hicho akiahidi kufanyia kazi sera za kuimarisha uchumi wa nchi hiyo. Akizungumza katika kikao kilichomalizika usiku wa manane, Ramaphosa amesema kupambana na rushwa sambamba na umaskini ni kipaumbele cha kwanza kwa chama chake. Amesema kuwa kikao cha kamati kuu […]

Uganda yaondoa kikomo cha umri wa kugombea urais

Wabunge wa Uganda wameyapitisha mabadiliko ya Katiba ambayo sasa yanamruhusu Rais wa sasa Yoweri Kaguta Museveni kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa kwa muhula wa sita. Baada ya siku tatu za majadiliano mazito na mivutano, hatimaye waondoa ukomo wa umri wa miaka 75 kwa mgombea urais. Wabunge wa upinzani walitoka ndani ya ukumbi zaidi ya […]

Korea Kusini yaitaka Marekani kusitisha mazoezi ya kijeshi nchini humo

Marekani na Korea Kaskazini zimekuwa katika mgogoro wa muda mrefu kufuatia mpango wa matumizi ya mabomu ya nyuklia unaofanywa na Korea Kaskazini. Michuano ya Olimpiki ya majira ya baridi inatarajiwa kuhusisha pia wanamichezo kutoka Korea Kaskazini jambo ambalo Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In anaeleza kuwa ni la kuimarisha uhusiano zaidi. Source: www.bbc.com

Wasambaza uongo Bakwata kukiona

BARAZA Kuu la Waislamu nchini (Bakwata) Mkoa wa Dar es Salaam limesema kuwa watu wote waliosambaza taarifa za uongo na uchochezi kuhusu Mufti na Shehe Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir pamoja na baraza hilo watachukuliwa hatua kwa kuwa wanafahamika. Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Shehe Mkuu wa Mkoa huo, Alhad Mussa […]

Reli ya Tanga-Arusha iliyokufa miaka 14 yafufuliwa

SERIKALI imesema imeanza kufufua reli ya kaskazini ya kutoka Tanga hadi Arusha, ambayo ilikufa miaka 14 iliyopita. Lengo la hatua hiyo ni kuwezesha wafanyabiashara na wananchi, kusafirisha mizigo yao kwa kutumia reli hiyo badala ya barabara, hatua itakayopunguza uharibifu wa miundombinu ya barabara nchini. Hayo yalisemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame […]

Magufuli: Four reasons why CCM won in 42 wards

Chama cha Mapinduzi (CCM) National Chairman Dr John Magufuli has outlined four reasons why the ruling party emerged the winner in the just ended councillorship race. Opening CCM’s 9th General Assembly in Dodoma, Monday morning, Dr Magufuli, who doubles as the President, said that the party won in 42 wards out of 43 in the […]

Jose Mourinho: Meneja wa Man Utd atakiwa kufafanua kuhusu Man City

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ametakiwa kufafanua aliyoyasema kabla ya bebi ya Jumapili ambapo walilazwa na Manchester City 2-1 uwanjani Old Trafford. Chama cha Soka England (FA) kimemtaka Mreno huyo kufafanua zaidi kuhusu aliyoyasema katika kikao cha kabla ya mechi Ijumaa akizungumza na wanahabari. Mourinho alidai wachezaji wa City huanguka kwa urahisi sana. Alisema: […]

Tanzania yaongeza maradufu panya buku wanaotambua TB

Tanzania inaongeza maradufu idadi ya panya buku wanaotumika kuutambua ugonjwa wa kifua kikuua. Panya hao hupewa mafunzo na wana uwezo wa kunusa kamasi za binaadamu na kutambua kwa haraka ugonjwa wa TB. Wana uwezo wa kutambua sampuli mia moja kwa muda usiozidi dakika 20. Tofuati na binaadamu – wataalamu wa maabara wanaotumia siku nne kuchunguza […]

Tanzania yajitenga na Trump kuhusu Jerusalem

Tanzania imesema haikubaliani na hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania kupitia taarifa imesema nchi hiyo inaunga mkono makubaliano ya kimataifa ambayo yanatambua haki ya watu wa Palestina kumiliki Mashariki mwa Jerusalem kama ilivyokuwa kwenye mpaka wa kabla […]