Matokeo ya kidato cha nne yawabeba wasichana katika ufaulu

Baraza la Mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya kidato cha nne iliyofanyika Novemba 2017 ambapo jumla ya watahiniwa 385,767 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2017 wakiwemo wasichana 198,036 (51.34%) na wavulana 187,731 (48.66%).

Kati ya watahiniwa 385,767 waliosajiliwa, watahiniwa wa shule walikuwa 323,332 na watahiniwa wa kujitegemea walikuwa 62,435. Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya watahiniwa wa shule waliofaulu vizuri kwa daraja la I – III katika mwaka 2017 ni 95,337 sawa na asilimia 30.15, wakiwemo wasichana 39,441 sawa na asilimia 24.65 na wavulana 55,896 sawa na asilimia 35.80.

Ufaulu wa watahiniwa wa shule katika masomo Civics, History, Geography, Kiswahili, English Language, Biology, Basic Mathematics na Commerce umepanda kwa kati ya asilimia 1.07 na 9.85 ikilinganishwa na mwaka 2016.

Ufaulu wa juu kabisa ni ule wa somo la Kiswahili ambapo asilimia 84.42 ya watahiniwa wote wa Shule waliofanya somo hilo wamefaulu. Ufaulu wa chini kabisa ni ule wa somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 19.19 ya watahiniwa wote wa Shule waliofanya somo hilo wamefaulu.

Shule 10 bora kitaifa zenye watahiniwa zaidi ya 40 ni kama ifuatavyo.

1.ST. Francis Girls

2. Feza Boys

3.Kemebos

4. Bethel SABS Girls

5. Anwarite Girls

6. Marian Girls

7. Canossa

8. Feza Girls

9. Marian Boys

10. Shamsiye Boys.

source: www.habarileo.co.tz